Back to results

The Open University of Tanzania

Kuchunguza Dhamira za Nyimbo za Siti Bint Saad

Abstract

dc:description.abstract

Utafiti huu umeshughulikia dhamira za nyimbo za Siti binti Saad. Ili kukamilisha lengo kuu, madhumuni mahususi mawili yalitimizwa. Madhumuni hayo yalihusu kuchunguza na kutathmini dhamira za nyimbo za Siti binti Saad na kubainisha mbinu za kisanii zilizotumiwa na msanii huyo katika kuibua dhamira. Mtafiti ametumia mbinu za uchambuzi wa kifasihi, usaili katika kukusanya data za utafiti. Mikabala ya kimaelezo na ule wakifasihi ndiyo iliyotumika katika kuchambua data za utafiti wetu.Kwa jumla, utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali yaliyoulizwa kutokana na madhumuni mahsusi yautafiti huu ambapo imedhihirika kwamba, nyimbo za Siti binti Saad zimeshehenidhamira za matabaka utamaduni na mapenzi.Pia imebainika kwamba mbinu za kisanaa zimetumika kujenga dhamira, miongoni mwa dhamira zilizoibuliwa na matabaka utamaduni na mapenzi. Mbinu za kisaniizilizotumika ni kama mbinu ya simulizi, takriri, tashbiha, tash-hisi, ishara, misemo na muingiliano wa tanzu. Mwishoni mwa utafiti, kumetolewa mapendekezo kwa ajili ya tafiti zijazobaadae katika uwanja wa nyimbo za Siti binti Saad katika vipengele vyengine vya fani na maudhui kama vile matumizi ya lugha kwa upana zaidi, muundo, falsafa, ujumbe na maadili, mtazamo na msimamo.

Degree

thesis:*
Level dc:type.qualificationlevel
masters
Grantor dc:publisher.institution
The Open University of Tanzania
Year dc:date.issued
2016

Author and committee

dc:creator, dc:contributor.*
Author dc:creator
  • khamis, Wahida Ameir

Subjects

dc:subject × 1

Rights

Language dc:language
en

Chain of custody

source
Harvested from
Open University of Tanzania
Base URL
repository.out.ac.tz/cgi/oai2
Last updated
2026-07-24
Source record
OAI-PMH GetRecord
citation

khamis, Wahida Ameir. Kuchunguza Dhamira za Nyimbo za Siti Bint Saad. masters thesis, The Open University of Tanzania, 2016.