The Open University of Tanzania
Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Ngoma ya Kibati Mkowa wa Kusini Pemba
Abstract
dc:description.abstractNyimbo za ngoma ya Kibati ni nyimbo maarufu sana visiwani Zanzibar. Asili ya nyimbo hizo ni kutoka kisiwani Pemba, katika Mkoa wa Kusini, Wilaya ya Mkoani katika kiambo cha Chokocho Michenzani. Nyimbo hizo zimekuwa maarufu sana na zinaendelea kupendwa kutwa kucha. Utafiti huu umefanywa, kuchunguza dhima zinazopatikana katika nyimbo hizo. Data zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na wa kidhamira. Nadharia ya dhima na kazi na Nadhariaya simiotiki, zilitumika katika kutimiza lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba, dhima zinazojitokeza katika nyimbo za ngoma ya Kibati zimeweza kuakisi hali halisi ya maisha ya Wazanzibari katika Nyanja zote za maisha Kisiaasa, kiutamaduni, Kiuchumi na Kijamii. Aidha matokeo ya utafiti yameaonesha kwamba, mbinu za kisanaa zilizotumiwa na watunzi wa nyimbo za ngoma ya Kibati zimesheheni mafumbo, taswira, semi pamoja na matumizi ya lugha ya ishara. Kwa mfano wimbo wa Samaki wa Pono, utamu wa Ndizi, Mkate wa Mayai, Danganyayo zote zimejaa matumuzi ya taswira, semi, ishara na mafumbo.
Degree
thesis:*- Level dc:type.qualificationlevel
- masters
- Grantor dc:publisher.institution
- The Open University of Tanzania
- Year dc:date.issued
- 2016
Author and committee
dc:creator, dc:contributor.*- Author dc:creator
-
- Rashid, Halima Saleh
Subjects
dc:subject × 1Rights
- Language dc:language
- en