The Open University of Tanzania
Uchambuzi wa Viangama Tamati Katika Lahaja ya Kitumbatu
Abstract
dc:description.abstractUtafiti huu umefanyika Unguja katika kisiwa cha Tumbatu, kwenye shehia nne ambazo ni Gomani, Uvivini, Mtakuja na Jongowe. Lengo kuu ni kuchambua viangama tamati katika lahaja ya kitumbatu. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya viangama ya Zwicky (1977). Data zimekusanywa kwa njia ya mahojiano na ushuhudiaji. Walengwa wa utafiti huu ni wazee, watu wa makamo na vijana. Kila shehia wamesailiwa watu 25 wa umri na jinsia tafauti na kufanyiwa usaili watu 100. Utafiti umetumia data simulizi ambapo mtafiti amefanya mahojiano na kushuhudia kwa kusikiliza mazungumzo kutoka mikusanyiko ya watu mbalimbali. Kwa upande wa uchambuzi wa data, mtafiti amechambua aina za viangama tamati, maumbo ya viangama tamati na kategoria za maneno ambazo ni viegemewa vya viangama tamati katika lahaja ya Kitumbatu. Matokeo ya utafiti huu, data zimeonesha kuwa lahaja ya Kitumbatu ina viangama tamati vyenye maumbo yafuatayo: viwakilishi, vivumishi, viunganishi, vitenzi na vielezi. Maumbo hayo yameegemezwa kwenye nomino, vitenzi, viunganishi, vihusishi na viwakilishi. Kwa upande wa mapendekezo mtafiti amependekeza ufanyike utafiti wa viangama tamati wa lahaja nyingine. Pia amependekeza ufanyike utafiti wa viangama awali katika Kiswahili cha mazungumzo. Vile vile amependekeza utafiti wa kazi za viangama ufanyike. Mwisho amependekeza ufanywe utafiti wa viangama katika lugha mbalimbali hasa za makabila ya Tanzania.
Degree
thesis:*- Level dc:type.qualificationlevel
- masters
- Grantor dc:publisher.institution
- The Open University of Tanzania
- Year dc:date.issued
- 2016
Author and committee
dc:creator, dc:contributor.*- Author dc:creator
-
- Adi, Mwanaidi Masoud
Subjects
dc:subject × 1Rights
- Language dc:language
- en