Back to results

The Open University of Tanzania

Muundo wa Kirai Nomino katika lahaja ya Kimakunduchi

Abstract

dc:description.abstract

Utafiti huu umechunguza muundo wa kirai nomino katika lahaja ya Kimakunduchi.Malengo ya utafiti yalikuwa ni kubainisha vipengele vya muundo wa kirai nomino katika lahaja ya Kimakunduchi; kuelezea utaratibu au mpangilio wa vipengele vya muundo wa kirai nomino na lengo la tatu; ni kujadili dhima za kisarufi za kirai nomino. Utafiti huu ulitumia mkabala wa kimaelezo katika kukusanya na kuchambua data, huku nadharia ya sarufi miundo virai na dhana yake maarufu ya eksibaa ikiongoza utafiti huu. Utafiti ulifanyika Makunduchi mkoa wa kusini Unguja na ulihusisha shehia tatu ambazo ni shehia ya Kiongoni, shehia ya Nganani na shehia ya Mzuri.Watafitiwa walikuwa ni wazungumzaji asilia wa lahaja ya Kimakunduchi. Watafitiwa hao walichaguliwa kwa kutumia usampulishaji kusudio ambao mtafiti anachagua sampuli kulingana na malengo maalumu. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia njia ya hojaji na uchunguzi makini kupitia shughuli za kijamii kwa mfano mwaka kogwa, sherehe za harusi, maziko na kadhalika. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala stahilifu ambao ni ule unaotumia maelezo kulingana na data zilizopatikana kutoka kwa watafitiwa. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya sarufi miundo virai na dhana yake maarufu ya eksibaa. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba muundo wa kirai nomino katika lahaja ya Kimakunduchi una sifa za kimuundo ambazo hazipo mbali na lahaja nyingine pamoja na Kiswahili sanifu. Vile vile muundo wa kirai nomino katika lahaja ya Kimakunduchi umeonekana kuwa sawa na ule wa lugha za Kibantu na lahaja za Kiswahili kama ilivyoonyeshwa na wataalamu tofauti.

Degree

thesis:*
Level dc:type.qualificationlevel
masters
Grantor dc:publisher.institution
The Open University of Tanzania
Year dc:date.issued
2017

Author and committee

dc:creator, dc:contributor.*
Author dc:creator
  • Bavuai, Asha Iddi

Subjects

dc:subject × 1

Rights

Language dc:language
en

Chain of custody

source
Harvested from
Open University of Tanzania
Base URL
repository.out.ac.tz/cgi/oai2
Last updated
2026-07-24
Source record
OAI-PMH GetRecord
citation

Bavuai, Asha Iddi. Muundo wa Kirai Nomino katika lahaja ya Kimakunduchi. masters thesis, The Open University of Tanzania, 2017.