Back to search

The Open University Of Tanzania

Mchango wa Mashairi ya Bi Madina Ali El-Buhriy Katika Arudhi ya Kiswahili Tanga

Abstract

dc:description.abstract

Utafiti huu ulilenga kuchunguza dhamira zinazojitokeza katika mashairi ya Bi Madina Ali El-Buhriy na namna tamatali za usemi zinavyosaidia kujenga dhamira hizo. Tumefikia malengo kwa kuibua dhamira kumi na mbili na kuchambua tamathali za usemi nane. Tasinifu hii ina sura kuu sita. Katika Sura ya Kwanza kuna utangulizi wa jumla, historia fupi ya Bi Madina Ali El-Buhriy, Usuli wa mada ya utafiti, Usuli wa tatizo la utafiti, Tatizo la utafiti, Nia kuu ya utafiti, Malengo maalumu ya utafiti, Maswali ya utafiti, Umuhimu wa utafiti, Eneo la utafiti. Sura ya Pili, kuna Uhakiki wa kazi za mashairi, Utafiti uliofanyika katika ushairi na hitimishi. Kuna mikabala ya kinadharia, Maana ya Nadharia, Ufafanuzi wa Nadharia. Sura ya Tatu, kuna maelezo juu ya mbinu na njia zilizotumiwa na mtafiti katika ukusanyaji wa data na zana za utafiti, Ratiba ya mtafiti, bajeti. Katika Sura ya Nne,kuna uwasilishaji wa matokeo ya utafiti, dhamira kumi na mbili zimejadiliwa; Dhamira ya kutenda na kutendewa mema, Dhamira ya utunzaji wa Mazingira,Dhamira ya Kuhamasisha wanawake katika utunzi wa mashairi,Dhamira ya umalaya katika jamii, Dhamira ya umuhimu wa Wazazi, Dhamira ya hulka za binadamu, Dhamira ya kumbukizi, Dhamira ya matatizo ya maji katika Jiji la Dar Es Salaam, Dhamira ya Rushwa, Dhamira ya mabomu ya Mbagala, Dhamira ya ugomvi/mafarakano. Katika Sura ya Tano, kuna matumizi ya fani, kipengele kilichopewa uzito ni; lugha, tamathali za usemi zimechambuliwa kulingana na muktadha wa utunzi wa mshairi, tashibiha, taswira, stiari, nidaa, takriri, tashihisi, ritifaa, kejeli. Sura ya sita kuna maoni na mapendekezo kwa ajili ya jamii na tafiti zijazo.

Degree

thesis:*
Level dc:type.qualificationlevel
masters
Grantor dc:publisher.institution
The Open University Of Tanzania
Year dc:date.issued
2015

Author and committee

dc:creator, dc:contributor.*
Author dc:creator
  • kaguo, Joyce

Subjects

dc:subject × 1

Rights

Language dc:language
en

Chain of custody

source
Harvested from
Open University of Tanzania
Base URL
repository.out.ac.tz/cgi/oai2
Last updated
2026-07-24
Source record
OAI-PMH GetRecord
citation

kaguo, Joyce. Mchango wa Mashairi ya Bi Madina Ali El-Buhriy Katika Arudhi ya Kiswahili Tanga. masters thesis, The Open University Of Tanzania, 2015.