{"id":{"repo_id":"ou-tanzania","oai_identifier":"oai:repository.out.ac.tz:912"},"canonical_url":"https://search.dev.ndltd.org/etd/ou-tanzania/oai:repository.out.ac.tz:912","repository":{"repo_id":"ou-tanzania","name":"Open University of Tanzania","base_url":"http://repository.out.ac.tz/cgi/oai2"},"display":{"title":"Kuchunguza Matumizi ya Methali katika Jamii ya Wanyiramba","abstract":"Tasnifu hii inahusu matumizi ya methali katika jamii ya Wanyiramba. Kutokana na utafiti uliofanywa ulilenga kuchunguza methali za Kinyiramba huundwaje na zina muundo gani. Pili, utafiti huo ulichunguza matumizi ya methali na nafasi yake katika kujenga na kuimarisha maadili katika jamii. Kutokana na utafiti uliofanywa kwa kutumia njia ya hojaji na ushiriki nafsi imebainika kwamba ingawa methali ziko katika jamii ya Wanyiramba na zinasemwa na kusikika na wanajamii lakini kuna tofauti za aina mbili katika matumizi yake. Tofauti ya kwanza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofanyiwa utafiti walishindwa kueleza maana ya methali hizo hata kama waliweza kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Tofati ya pili iliyojitokeza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watafitiwa walishindwa kueleza ni katika mazingira yapi methali hutumiwa ili iwasilishe ujumbe uliofichika katika maana yake. Utafiti huu ulibaini pia kuwa ugumu wa kutambua maana na matumizi ya methali unatokana na ukweli kwamba mambo haya mawili hutegemea msemaji wa methali ana dhamira gani na yuko katika mazingira yapi ya matumizi. Laiti kama mazingira yangezingatiwa matumizi ya methali yangeongezeka na maadili ya jamii yangeimarika zaidi. Hivyo utafiti huu unapendekeza kwamba methali zikusanywe ili idadi yake ijulikane, maana zake za msingi zijulikane na zipewe nafasi zaidi ya kutumiwa katika mikusanyiko ya hadhara na kampeni mbalimbali katika jamii ili ziweze kusambaa.","abstract_html":"Tasnifu hii inahusu matumizi ya methali katika jamii ya Wanyiramba. Kutokana na utafiti uliofanywa ulilenga kuchunguza methali za Kinyiramba huundwaje na zina muundo gani. Pili, utafiti huo ulichunguza matumizi ya methali na nafasi yake katika kujenga na kuimarisha maadili katika jamii. Kutokana na utafiti uliofanywa kwa kutumia njia ya hojaji na ushiriki nafsi imebainika kwamba ingawa methali ziko katika jamii ya Wanyiramba na zinasemwa na kusikika na wanajamii lakini kuna tofauti za aina mbili katika matumizi yake. Tofauti ya kwanza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofanyiwa utafiti walishindwa kueleza maana ya methali hizo hata kama waliweza kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Tofati ya pili iliyojitokeza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watafitiwa walishindwa kueleza ni katika mazingira yapi methali hutumiwa ili iwasilishe ujumbe uliofichika katika maana yake. Utafiti huu ulibaini pia kuwa ugumu wa kutambua maana na matumizi ya methali unatokana na ukweli kwamba mambo haya mawili hutegemea msemaji wa methali ana dhamira gani na yuko katika mazingira yapi ya matumizi. Laiti kama mazingira yangezingatiwa matumizi ya methali yangeongezeka na maadili ya jamii yangeimarika zaidi. Hivyo utafiti huu unapendekeza kwamba methali zikusanywe ili idadi yake ijulikane, maana zake za msingi zijulikane na zipewe nafasi zaidi ya kutumiwa katika mikusanyiko ya hadhara na kampeni mbalimbali katika jamii ili ziweze kusambaa.","abstract_has_math":false,"creators":["Mtesigwa, Grace Kidyagilla"],"institution":"The Open University of Tanzania","degree_name":null,"degree_level":"masters","degree_discipline":null,"degree_department":null,"school":null,"contributors":[],"advisors":[],"committee_chairs":[],"committee_members":[],"year":2013,"date_issued":"2013","date_published":"2013","updated_at":"2026-07-24T03:40:13Z","subjects":["490 Other languages"],"languages":["en"],"rights":[],"rights_urls":[],"identifier_entries":[]},"links":{"outbound_url":null,"outbound_label":null,"outbound_source":null},"metadata_groups":[{"id":"people","label":"People","entries":[{"key":"dc:creator","label":"Author","values":["Mtesigwa, Grace Kidyagilla"]}]},{"id":"academic_context","label":"Academic Context","entries":[{"key":"dc:date","label":"Dc Date","values":["2013"]},{"key":"dc:date.issued","label":"Date","values":["2013"]},{"key":"dc:publisher.department","label":"Dc Publisher Department","values":["Linguistics and Literary Studies"]},{"key":"dc:publisher.institution","label":"Dc Publisher Institution","values":["The Open University of Tanzania"]},{"key":"dc:relation.isreferencedby","label":"Dc Relation Isreferencedby","values":["http://repository.out.ac.tz/912/"]},{"key":"dc:type","label":"Dc Type","values":["Thesis"]},{"key":"dc:type.qualificationlevel","label":"Dc Type Qualificationlevel","values":["masters"]}]},{"id":"subjects_keywords","label":"Subjects and Keywords","entries":[{"key":"dc:subject","label":"Dc Subject","values":["490 Other languages"]}]},{"id":"language_rights","label":"Language and Rights","entries":[{"key":"dc:language","label":"Dc Language","values":["en"]}]},{"id":"identifiers","label":"Identifiers","entries":[{"key":"dc:identifier.uri","label":"Identifier URI","values":["http://repository.out.ac.tz/912/1/Grace_final.pdf"]}]},{"id":"additional","label":"Additional Metadata","entries":[{"key":"dc:description.abstract","label":"Abstract","values":["Tasnifu hii inahusu matumizi ya methali katika jamii ya Wanyiramba. Kutokana na utafiti uliofanywa ulilenga kuchunguza methali za Kinyiramba huundwaje na zina muundo gani. Pili, utafiti huo ulichunguza matumizi ya methali na nafasi yake katika kujenga na kuimarisha maadili katika jamii. Kutokana na utafiti uliofanywa kwa kutumia njia ya hojaji na ushiriki nafsi imebainika kwamba ingawa methali ziko katika jamii ya Wanyiramba na zinasemwa na kusikika na wanajamii lakini kuna tofauti za aina mbili katika matumizi yake. Tofauti ya kwanza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofanyiwa utafiti walishindwa kueleza maana ya methali hizo hata kama waliweza kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Tofati ya pili iliyojitokeza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watafitiwa walishindwa kueleza ni katika mazingira yapi methali hutumiwa ili iwasilishe ujumbe uliofichika katika maana yake. Utafiti huu ulibaini pia kuwa ugumu wa kutambua maana na matumizi ya methali unatokana na ukweli kwamba mambo haya mawili hutegemea msemaji wa methali ana dhamira gani na yuko katika mazingira yapi ya matumizi. Laiti kama mazingira yangezingatiwa matumizi ya methali yangeongezeka na maadili ya jamii yangeimarika zaidi. Hivyo utafiti huu unapendekeza kwamba methali zikusanywe ili idadi yake ijulikane, maana zake za msingi zijulikane na zipewe nafasi zaidi ya kutumiwa katika mikusanyiko ya hadhara na kampeni mbalimbali katika jamii ili ziweze kusambaa."]},{"key":"dc:format","label":"Dc Format","values":["application/pdf"]},{"key":"dc:title","label":"Title","values":["Kuchunguza Matumizi ya Methali katika Jamii ya Wanyiramba"]}]}],"canonical_facts":{"dc:creator":["Mtesigwa, Grace Kidyagilla"],"dc:date":["2013"],"dc:date.issued":["2013"],"dc:description.abstract":["Tasnifu hii inahusu matumizi ya methali katika jamii ya Wanyiramba. Kutokana na utafiti uliofanywa ulilenga kuchunguza methali za Kinyiramba huundwaje na zina muundo gani. Pili, utafiti huo ulichunguza matumizi ya methali na nafasi yake katika kujenga na kuimarisha maadili katika jamii. Kutokana na utafiti uliofanywa kwa kutumia njia ya hojaji na ushiriki nafsi imebainika kwamba ingawa methali ziko katika jamii ya Wanyiramba na zinasemwa na kusikika na wanajamii lakini kuna tofauti za aina mbili katika matumizi yake. Tofauti ya kwanza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofanyiwa utafiti walishindwa kueleza maana ya methali hizo hata kama waliweza kuzitafsiri kwa lugha ya Kiswahili. Tofati ya pili iliyojitokeza ni kwamba zaidi ya nusu ya idadi ya watafitiwa walishindwa kueleza ni katika mazingira yapi methali hutumiwa ili iwasilishe ujumbe uliofichika katika maana yake. Utafiti huu ulibaini pia kuwa ugumu wa kutambua maana na matumizi ya methali unatokana na ukweli kwamba mambo haya mawili hutegemea msemaji wa methali ana dhamira gani na yuko katika mazingira yapi ya matumizi. Laiti kama mazingira yangezingatiwa matumizi ya methali yangeongezeka na maadili ya jamii yangeimarika zaidi. Hivyo utafiti huu unapendekeza kwamba methali zikusanywe ili idadi yake ijulikane, maana zake za msingi zijulikane na zipewe nafasi zaidi ya kutumiwa katika mikusanyiko ya hadhara na kampeni mbalimbali katika jamii ili ziweze kusambaa."],"dc:format":["application/pdf"],"dc:identifier.uri":["http://repository.out.ac.tz/912/1/Grace_final.pdf"],"dc:language":["en"],"dc:publisher.department":["Linguistics and Literary Studies"],"dc:publisher.institution":["The Open University of Tanzania"],"dc:relation.isreferencedby":["http://repository.out.ac.tz/912/"],"dc:subject":["490 Other languages"],"dc:title":["Kuchunguza Matumizi ya Methali katika Jamii ya Wanyiramba"],"dc:type":["Thesis"],"dc:type.qualificationlevel":["masters"]},"updated_at":"2026-07-24T03:40:13Z"}