Back to results

The Open University of Tanzania

Kuchunguza Tamathali za Usemi katika Mashairi ya Magazetini: Uchunguzi kifani wa Mashairi ya UKIMWI katika Magazeti ya Kiswahili

Abstract

dc:description.abstract

Utafiti huu umeshughulikia matumizi ya lugha ya tamathali za usemi katika mashairi ya magazetini. Ili kukamilisha lengo hili kuu madhumuni mahususi matatu yalitimizwa. Madhumuni hayo yalihusu kubainisha tamathali za usemi, dhamira na dhima za tamathali za usemi katika kujenga dhamira mbalimbali katika mashairi ya magazetini. Mtafiti ametumia mbinu za uchambuzi wa kimaudhui, usaili na upitiaji wa nyaraka katika kukusanya data za utafiti. Mikabala ya kifasihi na ule wa kimaelezo ndio iliyotumika katika kuchambua data za utafiti wetu. Kwa ujumla utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali ya utafiti wetu ambapo imethihirika kwamba, mashairi ya magazetini yamesheheni matumizi ya tamathali mbalimbali za usemi. Pia imebainika kwamba tamathali hizo za usemi zinatumika kujenga dhamira mbalimbali na mwisho tamathali za usemi zimebainika kuwa na dhima mbalimbali za kifani na kimaudhui katika kujenga na kuwasilisha dhamira mbalimbali kuhusiana na masuala ya UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania. Mwishoni mwa utafiti kumetolewa mapendekezo kwa wadau mbalimbali wa mashairi ya magazetini kuhusiana na namna bora za kuimarisha mashairi hayo ili yaendelee kutekeleza wajibu wake kwa jamii. Pia, tumetoa mapendekezo kwa ajili ya tafiti za baadaye katika uwanja wa mashairi ya magazetini.

Degree

thesis:*
Level dc:type.qualificationlevel
masters
Grantor dc:publisher.institution
The Open University of Tanzania
Year dc:date.issued
2014

Author and committee

dc:creator, dc:contributor.*
Author dc:creator
  • Kombo, Omari Mtunguja

Subjects

dc:subject × 1

Rights

Language dc:language
en

Chain of custody

source
Harvested from
Open University of Tanzania
Base URL
repository.out.ac.tz/cgi/oai2
Last updated
2026-07-24
Source record
OAI-PMH GetRecord
citation

Kombo, Omari Mtunguja. Kuchunguza Tamathali za Usemi katika Mashairi ya Magazetini: Uchunguzi kifani wa Mashairi ya UKIMWI katika Magazeti ya Kiswahili. masters thesis, The Open University of Tanzania, 2014.