{"id":{"repo_id":"ou-tanzania","oai_identifier":"oai:repository.out.ac.tz:1841"},"canonical_url":"https://search.dev.ndltd.org/etd/ou-tanzania/oai:repository.out.ac.tz:1841","repository":{"repo_id":"ou-tanzania","name":"Open University of Tanzania","base_url":"http://repository.out.ac.tz/cgi/oai2"},"display":{"title":"Kutathmini Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa","abstract":"Diwani ya Howani Mwana Howani ni Diwani ambayo imekusanya tenzi mbili ambazo ni Howani na Mwana Kukuwa.Tenzi hizo zinazungumzia mila na desturi za Mwanamke wa Visiwani kuanzia alipobeba ujauzito mpaka alipoolewa na kupelekwa kwake. Hivyo katika utafiti huu mtafiti alichunguza vipengele vya fani kama vile: matumizi ya lugha, mandhari na wahusika ili kuona ni jinsi gani mila na desturi za mwanamke wa visiwani zilivyojidhihirisha katika tenzi teule. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Wateuliwa wa utafiti huu waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi lengwa. Aidha, data zilizokusanywa katika utafiti huu, zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegunduwa kuwa tenzi za Howani na Mwana Kukuwa zimejedili kwa kiasi kikubwa mila na desturi za mwanamke wa visiwani. Mila na desturi hizo zimeanzia tokea mwanamke alipokuwa mja mzito, kipindi cha kujifunguwa, malezi ya mtoto wa kike, kipindi cha kubaleghe, kipindi cha ndoa, katika mavazi, mapambo, ngoma za asili, pamoja na tiba za asili. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Sosholojia katika kuelezea lengo mahsusi la kwanza na la pili na Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kuchambua data zinazohusiana na lengo mahsusi la tatu, ili kufikia lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa vipengele kama vile mandhari, matumizi ya lugha pamoja na wahusika vimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika tenzi za Howani na Mwana Kukuwa, vipengele hivyo vimesaidia sana katika kufikisha malengo ya Mwandishi ya kuelezea Mila na Desturi za mwanamke katika jamii ya visiwani Zanzibar.","abstract_html":"Diwani ya Howani Mwana Howani ni Diwani ambayo imekusanya tenzi mbili ambazo ni Howani na Mwana Kukuwa.Tenzi hizo zinazungumzia mila na desturi za Mwanamke wa Visiwani kuanzia alipobeba ujauzito mpaka alipoolewa na kupelekwa kwake. Hivyo katika utafiti huu mtafiti alichunguza vipengele vya fani kama vile: matumizi ya lugha, mandhari na wahusika ili kuona ni jinsi gani mila na desturi za mwanamke wa visiwani zilivyojidhihirisha katika tenzi teule. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Wateuliwa wa utafiti huu waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi lengwa. Aidha, data zilizokusanywa katika utafiti huu, zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegunduwa kuwa tenzi za Howani na Mwana Kukuwa zimejedili kwa kiasi kikubwa mila na desturi za mwanamke wa visiwani. Mila na desturi hizo zimeanzia tokea mwanamke alipokuwa mja mzito, kipindi cha kujifunguwa, malezi ya mtoto wa kike, kipindi cha kubaleghe, kipindi cha ndoa, katika mavazi, mapambo, ngoma za asili, pamoja na tiba za asili. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Sosholojia katika kuelezea lengo mahsusi la kwanza na la pili na Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kuchambua data zinazohusiana na lengo mahsusi la tatu, ili kufikia lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa vipengele kama vile mandhari, matumizi ya lugha pamoja na wahusika vimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika tenzi za Howani na Mwana Kukuwa, vipengele hivyo vimesaidia sana katika kufikisha malengo ya Mwandishi ya kuelezea Mila na Desturi za mwanamke katika jamii ya visiwani Zanzibar.","abstract_has_math":false,"creators":["Mohamed, Fatma Ali"],"institution":"The Open University of Tanzania","degree_name":null,"degree_level":"masters","degree_discipline":null,"degree_department":null,"school":null,"contributors":[],"advisors":[],"committee_chairs":[],"committee_members":[],"year":2016,"date_issued":"2016","date_published":"2016","updated_at":"2026-07-24T03:40:45Z","subjects":["490 Other languages"],"languages":["en"],"rights":[],"rights_urls":[],"identifier_entries":[]},"links":{"outbound_url":null,"outbound_label":null,"outbound_source":null},"metadata_groups":[{"id":"people","label":"People","entries":[{"key":"dc:creator","label":"Author","values":["Mohamed, Fatma Ali"]}]},{"id":"academic_context","label":"Academic Context","entries":[{"key":"dc:date","label":"Dc Date","values":["2016"]},{"key":"dc:date.issued","label":"Date","values":["2016"]},{"key":"dc:publisher.department","label":"Dc Publisher Department","values":["Linguistics and Literary Studies"]},{"key":"dc:publisher.institution","label":"Dc Publisher Institution","values":["The Open University of Tanzania"]},{"key":"dc:relation.isreferencedby","label":"Dc Relation Isreferencedby","values":["http://repository.out.ac.tz/1841/"]},{"key":"dc:type","label":"Dc Type","values":["Thesis"]},{"key":"dc:type.qualificationlevel","label":"Dc Type Qualificationlevel","values":["masters"]}]},{"id":"subjects_keywords","label":"Subjects and Keywords","entries":[{"key":"dc:subject","label":"Dc Subject","values":["490 Other languages"]}]},{"id":"language_rights","label":"Language and Rights","entries":[{"key":"dc:language","label":"Dc Language","values":["en"]}]},{"id":"identifiers","label":"Identifiers","entries":[{"key":"dc:identifier.uri","label":"Identifier URI","values":["http://repository.out.ac.tz/1841/1/UTAFITI_-_FKM_FINAL-_HABIBA.pdf"]}]},{"id":"additional","label":"Additional Metadata","entries":[{"key":"dc:description.abstract","label":"Abstract","values":["Diwani ya Howani Mwana Howani ni Diwani ambayo imekusanya tenzi mbili ambazo ni Howani na Mwana Kukuwa.Tenzi hizo zinazungumzia mila na desturi za Mwanamke wa Visiwani kuanzia alipobeba ujauzito mpaka alipoolewa na kupelekwa kwake. Hivyo katika utafiti huu mtafiti alichunguza vipengele vya fani kama vile: matumizi ya lugha, mandhari na wahusika ili kuona ni jinsi gani mila na desturi za mwanamke wa visiwani zilivyojidhihirisha katika tenzi teule. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Wateuliwa wa utafiti huu waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi lengwa. Aidha, data zilizokusanywa katika utafiti huu, zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegunduwa kuwa tenzi za Howani na Mwana Kukuwa zimejedili kwa kiasi kikubwa mila na desturi za mwanamke wa visiwani. Mila na desturi hizo zimeanzia tokea mwanamke alipokuwa mja mzito, kipindi cha kujifunguwa, malezi ya mtoto wa kike, kipindi cha kubaleghe, kipindi cha ndoa, katika mavazi, mapambo, ngoma za asili, pamoja na tiba za asili. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Sosholojia katika kuelezea lengo mahsusi la kwanza na la pili na Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kuchambua data zinazohusiana na lengo mahsusi la tatu, ili kufikia lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa vipengele kama vile mandhari, matumizi ya lugha pamoja na wahusika vimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika tenzi za Howani na Mwana Kukuwa, vipengele hivyo vimesaidia sana katika kufikisha malengo ya Mwandishi ya kuelezea Mila na Desturi za mwanamke katika jamii ya visiwani Zanzibar."]},{"key":"dc:format","label":"Dc Format","values":["application/pdf"]},{"key":"dc:title","label":"Title","values":["Kutathmini Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa"]}]}],"canonical_facts":{"dc:creator":["Mohamed, Fatma Ali"],"dc:date":["2016"],"dc:date.issued":["2016"],"dc:description.abstract":["Diwani ya Howani Mwana Howani ni Diwani ambayo imekusanya tenzi mbili ambazo ni Howani na Mwana Kukuwa.Tenzi hizo zinazungumzia mila na desturi za Mwanamke wa Visiwani kuanzia alipobeba ujauzito mpaka alipoolewa na kupelekwa kwake. Hivyo katika utafiti huu mtafiti alichunguza vipengele vya fani kama vile: matumizi ya lugha, mandhari na wahusika ili kuona ni jinsi gani mila na desturi za mwanamke wa visiwani zilivyojidhihirisha katika tenzi teule. Utafiti huu ulitumia mbinu ya maktabani. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Wateuliwa wa utafiti huu waliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi lengwa. Aidha, data zilizokusanywa katika utafiti huu, zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegunduwa kuwa tenzi za Howani na Mwana Kukuwa zimejedili kwa kiasi kikubwa mila na desturi za mwanamke wa visiwani. Mila na desturi hizo zimeanzia tokea mwanamke alipokuwa mja mzito, kipindi cha kujifunguwa, malezi ya mtoto wa kike, kipindi cha kubaleghe, kipindi cha ndoa, katika mavazi, mapambo, ngoma za asili, pamoja na tiba za asili. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Sosholojia katika kuelezea lengo mahsusi la kwanza na la pili na Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kuchambua data zinazohusiana na lengo mahsusi la tatu, ili kufikia lengo la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa vipengele kama vile mandhari, matumizi ya lugha pamoja na wahusika vimejitokeza kwa kiasi kikubwa katika tenzi za Howani na Mwana Kukuwa, vipengele hivyo vimesaidia sana katika kufikisha malengo ya Mwandishi ya kuelezea Mila na Desturi za mwanamke katika jamii ya visiwani Zanzibar."],"dc:format":["application/pdf"],"dc:identifier.uri":["http://repository.out.ac.tz/1841/1/UTAFITI_-_FKM_FINAL-_HABIBA.pdf"],"dc:language":["en"],"dc:publisher.department":["Linguistics and Literary Studies"],"dc:publisher.institution":["The Open University of Tanzania"],"dc:relation.isreferencedby":["http://repository.out.ac.tz/1841/"],"dc:subject":["490 Other languages"],"dc:title":["Kutathmini Mila na Desturi za Mwanamke wa Visiwani katika Tenzi za Howani na Mwana Kukuwa"],"dc:type":["Thesis"],"dc:type.qualificationlevel":["masters"]},"updated_at":"2026-07-24T03:40:45Z"}