{"id":{"repo_id":"ou-tanzania","oai_identifier":"oai:repository.out.ac.tz:1400"},"canonical_url":"https://search.dev.ndltd.org/etd/ou-tanzania/oai:repository.out.ac.tz:1400","repository":{"repo_id":"ou-tanzania","name":"Open University of Tanzania","base_url":"http://repository.out.ac.tz/cgi/oai2"},"display":{"title":"Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba","abstract":"Utafiti huu ulikuwa na lengo la “Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba katika Muktadha wa Harusini, Msibani, Uvuvini na Kilimoni”. Malengo ya utafiti yalikuwa; (i) Kuainisha msamiati wa harusini, msibani, uvuvini na kilimoni unaotumika katika lahaja ya Kipemba. (ii) Kutathmini tofauti ya kiasi cha mabadiliko ya matumizi ya msamiati huo. na (iii) kuchunguza sababu zilizosababisha mabadiliko ya matumizi ya msamiati wa Kipemba. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Foucault (1981) ya Mwenendo na Mabadiliko. Nadharia ya Darwin (1838) ya Ubadilikaji na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM) ya Giles ya mwaka (1991). Jumla ya watafitiwa 87 walishiriki katika utafiti huu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, usaili na maelezo. Pia data ziliainishwa kwa njia ya kiidadi (kitakwimu) na isiyo ya kiidadi (maelezo). Utafiti umeonesha kuwa; (i) Msamiati wa muktadha wa harusini umebadilika zaidi kuliko miktadha mingine mitatu sawa na 33.33%. (ii) Msamiati wa kilimoni na uvuvini ukifuatia sawa na 22.81% kwa kila muktadha. (iii) Utafiti umegundua kuwa msamiati wa msibani umebadilika kwa kiwango kidogo wastani wa 21.05%. Sababu za mabadiliko hayo tafiti imeonesha ni kukua kwa sayansi na teknolojia, matumizi ya utandawazi pamoja na vyombo vya mawasiliano, kuwepo kwa lahaja iliyorasmi, athari ya maendeleo ya watu kuhamahama, mabadiliko ya kiutamaduni, maingiliano ya kindoa na misimamo ya kidini. Utafiti huu unapendekeza, msamiati wa Kipemba uendelee kutumika kwani unasaidia kuwatambua watu wenye asili hiyo na kujaza pengo la istilahi za Kiswahili na msamiati wa Kipemba ni amana na hazina ya lugha yetu uhifadhiwe vizuri ili amana hii ya lugha isipotee.","abstract_html":"Utafiti huu ulikuwa na lengo la “Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba katika Muktadha wa Harusini, Msibani, Uvuvini na Kilimoni”. Malengo ya utafiti yalikuwa; (i) Kuainisha msamiati wa harusini, msibani, uvuvini na kilimoni unaotumika katika lahaja ya Kipemba. (ii) Kutathmini tofauti ya kiasi cha mabadiliko ya matumizi ya msamiati huo. na (iii) kuchunguza sababu zilizosababisha mabadiliko ya matumizi ya msamiati wa Kipemba. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Foucault (1981) ya Mwenendo na Mabadiliko. Nadharia ya Darwin (1838) ya Ubadilikaji na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM) ya Giles ya mwaka (1991). Jumla ya watafitiwa 87 walishiriki katika utafiti huu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, usaili na maelezo. Pia data ziliainishwa kwa njia ya kiidadi (kitakwimu) na isiyo ya kiidadi (maelezo). Utafiti umeonesha kuwa; (i) Msamiati wa muktadha wa harusini umebadilika zaidi kuliko miktadha mingine mitatu sawa na 33.33%. (ii) Msamiati wa kilimoni na uvuvini ukifuatia sawa na 22.81% kwa kila muktadha. (iii) Utafiti umegundua kuwa msamiati wa msibani umebadilika kwa kiwango kidogo wastani wa 21.05%. Sababu za mabadiliko hayo tafiti imeonesha ni kukua kwa sayansi na teknolojia, matumizi ya utandawazi pamoja na vyombo vya mawasiliano, kuwepo kwa lahaja iliyorasmi, athari ya maendeleo ya watu kuhamahama, mabadiliko ya kiutamaduni, maingiliano ya kindoa na misimamo ya kidini. Utafiti huu unapendekeza, msamiati wa Kipemba uendelee kutumika kwani unasaidia kuwatambua watu wenye asili hiyo na kujaza pengo la istilahi za Kiswahili na msamiati wa Kipemba ni amana na hazina ya lugha yetu uhifadhiwe vizuri ili amana hii ya lugha isipotee.","abstract_has_math":false,"creators":["Suleiman, Kauthar Abdalla"],"institution":"The Open University Of Tanzania","degree_name":null,"degree_level":"masters","degree_discipline":null,"degree_department":null,"school":null,"contributors":[],"advisors":[],"committee_chairs":[],"committee_members":[],"year":2015,"date_issued":"2015","date_published":"2015","updated_at":"2026-07-24T03:40:33Z","subjects":["490 Other languages"],"languages":["en"],"rights":[],"rights_urls":[],"identifier_entries":[]},"links":{"outbound_url":null,"outbound_label":null,"outbound_source":null},"metadata_groups":[{"id":"people","label":"People","entries":[{"key":"dc:creator","label":"Author","values":["Suleiman, Kauthar Abdalla"]}]},{"id":"academic_context","label":"Academic Context","entries":[{"key":"dc:date","label":"Dc Date","values":["2015"]},{"key":"dc:date.issued","label":"Date","values":["2015"]},{"key":"dc:publisher.department","label":"Dc Publisher Department","values":["Linguistics and Literary studies"]},{"key":"dc:publisher.institution","label":"Dc Publisher Institution","values":["The Open University Of Tanzania"]},{"key":"dc:relation.isreferencedby","label":"Dc Relation Isreferencedby","values":["http://repository.out.ac.tz/1400/"]},{"key":"dc:type","label":"Dc Type","values":["Thesis"]},{"key":"dc:type.qualificationlevel","label":"Dc Type Qualificationlevel","values":["masters"]}]},{"id":"subjects_keywords","label":"Subjects and Keywords","entries":[{"key":"dc:subject","label":"Dc Subject","values":["490 Other languages"]}]},{"id":"language_rights","label":"Language and Rights","entries":[{"key":"dc:language","label":"Dc Language","values":["en"]}]},{"id":"identifiers","label":"Identifiers","entries":[{"key":"dc:identifier.uri","label":"Identifier URI","values":["http://repository.out.ac.tz/1400/1/KAUTHAR_ABDALLA_SULEIMAN_.pdf"]}]},{"id":"additional","label":"Additional Metadata","entries":[{"key":"dc:description.abstract","label":"Abstract","values":["Utafiti huu ulikuwa na lengo la “Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba katika Muktadha wa Harusini, Msibani, Uvuvini na Kilimoni”. Malengo ya utafiti yalikuwa; (i) Kuainisha msamiati wa harusini, msibani, uvuvini na kilimoni unaotumika katika lahaja ya Kipemba. (ii) Kutathmini tofauti ya kiasi cha mabadiliko ya matumizi ya msamiati huo. na (iii) kuchunguza sababu zilizosababisha mabadiliko ya matumizi ya msamiati wa Kipemba. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Foucault (1981) ya Mwenendo na Mabadiliko. Nadharia ya Darwin (1838) ya Ubadilikaji na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM) ya Giles ya mwaka (1991). Jumla ya watafitiwa 87 walishiriki katika utafiti huu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, usaili na maelezo. Pia data ziliainishwa kwa njia ya kiidadi (kitakwimu) na isiyo ya kiidadi (maelezo). Utafiti umeonesha kuwa; (i) Msamiati wa muktadha wa harusini umebadilika zaidi kuliko miktadha mingine mitatu sawa na 33.33%. (ii) Msamiati wa kilimoni na uvuvini ukifuatia sawa na 22.81% kwa kila muktadha. (iii) Utafiti umegundua kuwa msamiati wa msibani umebadilika kwa kiwango kidogo wastani wa 21.05%. Sababu za mabadiliko hayo tafiti imeonesha ni kukua kwa sayansi na teknolojia, matumizi ya utandawazi pamoja na vyombo vya mawasiliano, kuwepo kwa lahaja iliyorasmi, athari ya maendeleo ya watu kuhamahama, mabadiliko ya kiutamaduni, maingiliano ya kindoa na misimamo ya kidini. Utafiti huu unapendekeza, msamiati wa Kipemba uendelee kutumika kwani unasaidia kuwatambua watu wenye asili hiyo na kujaza pengo la istilahi za Kiswahili na msamiati wa Kipemba ni amana na hazina ya lugha yetu uhifadhiwe vizuri ili amana hii ya lugha isipotee."]},{"key":"dc:format","label":"Dc Format","values":["application/pdf"]},{"key":"dc:title","label":"Title","values":["Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba"]}]}],"canonical_facts":{"dc:creator":["Suleiman, Kauthar Abdalla"],"dc:date":["2015"],"dc:date.issued":["2015"],"dc:description.abstract":["Utafiti huu ulikuwa na lengo la “Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba katika Muktadha wa Harusini, Msibani, Uvuvini na Kilimoni”. Malengo ya utafiti yalikuwa; (i) Kuainisha msamiati wa harusini, msibani, uvuvini na kilimoni unaotumika katika lahaja ya Kipemba. (ii) Kutathmini tofauti ya kiasi cha mabadiliko ya matumizi ya msamiati huo. na (iii) kuchunguza sababu zilizosababisha mabadiliko ya matumizi ya msamiati wa Kipemba. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Foucault (1981) ya Mwenendo na Mabadiliko. Nadharia ya Darwin (1838) ya Ubadilikaji na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano (NKM) ya Giles ya mwaka (1991). Jumla ya watafitiwa 87 walishiriki katika utafiti huu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji, usaili na maelezo. Pia data ziliainishwa kwa njia ya kiidadi (kitakwimu) na isiyo ya kiidadi (maelezo). Utafiti umeonesha kuwa; (i) Msamiati wa muktadha wa harusini umebadilika zaidi kuliko miktadha mingine mitatu sawa na 33.33%. (ii) Msamiati wa kilimoni na uvuvini ukifuatia sawa na 22.81% kwa kila muktadha. (iii) Utafiti umegundua kuwa msamiati wa msibani umebadilika kwa kiwango kidogo wastani wa 21.05%. Sababu za mabadiliko hayo tafiti imeonesha ni kukua kwa sayansi na teknolojia, matumizi ya utandawazi pamoja na vyombo vya mawasiliano, kuwepo kwa lahaja iliyorasmi, athari ya maendeleo ya watu kuhamahama, mabadiliko ya kiutamaduni, maingiliano ya kindoa na misimamo ya kidini. Utafiti huu unapendekeza, msamiati wa Kipemba uendelee kutumika kwani unasaidia kuwatambua watu wenye asili hiyo na kujaza pengo la istilahi za Kiswahili na msamiati wa Kipemba ni amana na hazina ya lugha yetu uhifadhiwe vizuri ili amana hii ya lugha isipotee."],"dc:format":["application/pdf"],"dc:identifier.uri":["http://repository.out.ac.tz/1400/1/KAUTHAR_ABDALLA_SULEIMAN_.pdf"],"dc:language":["en"],"dc:publisher.department":["Linguistics and Literary studies"],"dc:publisher.institution":["The Open University Of Tanzania"],"dc:relation.isreferencedby":["http://repository.out.ac.tz/1400/"],"dc:subject":["490 Other languages"],"dc:title":["Kuchunguza Kiwango cha Mabadiliko ya Matumizi ya Msamiati wa Kipemba"],"dc:type":["Thesis"],"dc:type.qualificationlevel":["masters"]},"updated_at":"2026-07-24T03:40:33Z"}