Back to results

The Open University Of Tanzania

Kuchunguza Sifa za Kifani za Utendi wa Kiswahili: Mfano Utendi wa Fumo Liyongo

Abstract

dc:description.abstract

Utafiti huu unahusu kuchunguza sifa za kifani za Utendi au Utenzi wa Kiswahili. Utafiti huu ulichunguza vipengele vya fani kama vile; muundo, mtindo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha katika Utendi wa Kiswahili. Mfano, Utendi wa Fumo Liyongo, ili, kuona ni jinsi gani sifa za kifani zinavyojidhihirisha katika tenzi za Kiswahili. Utafiti huu ulitumia mbinu ya Maktaba. Wateuliwa wa utafiti huu walipatikana kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalumu. Aidha, data za utafiti huu zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya kimaelezo. Utafiti huu umegundua kuwa tenzi za Kiswahili, zina sifa za kifani mahususi. Utafiti huu umegundua kuwa, neno na dhana tenzi ni sawa na tendi miongoni mwa jamii za Waswahili. Aidha, utafiti umegundua kuwa, tenzi za Kiswahili, zina sifa za kifani zinazofanana. Kwa mfano, zote zina mianzo na miishio inayofanana, ya kuanza kwa duwa na kumaliziya kwa duwa. Huwa na muundo na mtindo wa baharu ya Utendi. Utenzi, huweza kuwapo au kutakuwapo mhusika shujaa. Aidha, utafiti umegundua kuwa, tenzi za Kiswahili, hazia urefu mahususi au idadi maalumu ya beti. Sifa nyengine ni uunganifu na mapisi ya kweli. Pia, huwa una maudhui makubwa ya Dini ya Kiislamu. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Umuundo na Nadharia ya Ujumi wa Kiafrika katika kufikisha lengo lake.

Degree

thesis:*
Level dc:type.qualificationlevel
masters
Grantor dc:publisher.institution
The Open University Of Tanzania
Year dc:date.issued
2015

Author and committee

dc:creator, dc:contributor.*
Author dc:creator
  • Faki, Ali Mussa

Subjects

dc:subject × 1

Rights

Language dc:language
en

Chain of custody

source
Harvested from
Open University of Tanzania
Base URL
repository.out.ac.tz/cgi/oai2
Last updated
2026-07-24
Source record
OAI-PMH GetRecord
citation

Faki, Ali Mussa. Kuchunguza Sifa za Kifani za Utendi wa Kiswahili: Mfano Utendi wa Fumo Liyongo. masters thesis, The Open University Of Tanzania, 2015.