Back to search

The Open University of Tanzania

Changamoto za Kutumia Istilahi Mbili kwa Dhana Moja Katika Kufundisha Isimu na Fasihi Shule za Sekondari: Mfano Kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Tanzania

Abstract

dc:description.abstract

Utafiti huu umeshughulikia changamoto za kutumia istilahi mbili kwa dhana moja katika kufundisha isimu na fasihi shule za sekondari za Tanzania. Lengo la utafiti huu ni kuchunguza matumizi ya istilahi mbili kwa dhana moja katika kufundisha isimu na fasihi ya Kiswahili kwa shule za sekondari, kudadisi usuli wake na kupendekeza njia za kuondokana na tatizo hili. Utafiti huu umetumia muundo wa kimaelezo na mbinu ya usampulishaji iliyotumika ni usampulishaji nasibu tabakishi na umefanywa katika baadhi ya shule za mkoa wa kusini Pemba. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni mbinu ya dodoso. Kuhusu matokeo ya utafiti imebainika kwamba kuna matumizi makubwa ya istilahi mbili kwa dhana katika shule za sekondari katika kufundisha isimu na fasihi ya Kiswahili. Hali hii imesababisha wanafunzi kukanganyikiwa, kufeli na hata kulichukia somo. Kwa hivyo matumizi ya istilahi mbili kwa dhana moja ni dhahiri kuwa huathiri ujifunzaji wa isimu na fasihi ya Kiswahili. Mapendekezo yanayotokana na utafiti huu ni pamoja na kuanzisha vitengo vya kuunda na kusimamia matumizi ya istilahi kwa ujumla.

Degree

thesis:*
Level dc:type.qualificationlevel
masters
Grantor dc:publisher.institution
The Open University of Tanzania
Year dc:date.issued
2016

Author and committee

dc:creator, dc:contributor.*
Author dc:creator
  • Abdalla, Saleh Ali

Subjects

dc:subject × 1

Rights

Language dc:language
en

Chain of custody

source
Harvested from
Open University of Tanzania
Base URL
repository.out.ac.tz/cgi/oai2
Last updated
2026-07-24
Source record
OAI-PMH GetRecord
citation

Abdalla, Saleh Ali. Changamoto za Kutumia Istilahi Mbili kwa Dhana Moja Katika Kufundisha Isimu na Fasihi Shule za Sekondari: Mfano Kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, Tanzania. masters thesis, The Open University of Tanzania, 2016.