The Open University Of Tanzania
Itikadi katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo: Utafiti Linganishi wa Ngoma ya Ng’wanamalundi na Fumo Liongo
Abstract
dc:description.abstractKazi hii ilihusika na mada inayohusiana na Kuchunguza mbinu za kitanzia za Ki-Aristotle katika Tamthiliya za Fumo Liongo na Sundiata. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni kuchambua matumizi ya mbinu za tanzia za Kiaristotle katika tamthiliya ya Fumo Liongo na Sundiata, kuelezea matumizi ya mbinu ambazo si za tanzia za Ki-Aristotle katika tamthiliya teule na kuchambua dhamira katika tamthiliya za Fumo Liongo na Sundiata. Data za utafiti zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya tanzia ya Ki-Aristotle. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa, mbinu za Ki-Aristotle zinazojitokeza katika tamthiliya teule ni msuko, wahusika, dhamira, fikra, utumiaji wa jukwaa na mtungo wa tamthiliya. Mbinu zisizo za Ki-Aristotle ni utendi, usimuliaji, diolojia, monolojia, majigambo na kuchanganya ushairi na nathari. Kwa upande wa dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya teule ni uongozi kandamizi, rushwa katika jamii, usaliti, matabaka, nafasi ya mwanamke na ushirikina katika jamii.
Degree
thesis:*- Level dc:type.qualificationlevel
- masters
- Grantor dc:publisher.institution
- The Open University Of Tanzania
- Year dc:date.issued
- 2015
Author and committee
dc:creator, dc:contributor.*- Author dc:creator
-
- Mhangilwa, Salome Clemence
Subjects
dc:subject × 1Rights
- Language dc:language
- en